Saturday, September 10, 2016VIPODOZI
Vipodozi ni mchanganyiko wa kemikali mbalimbali ambazo hutengenezwa ili kurutubisha hali ya ngozi. Vipodozi vipo katika namna tofautitofauti mfano, inaweza kuwa katika hali ya kimiminika, katika hali ya gesi ama katika hali ya (solid).
-         Vipo vipodozi ambavyo vimeruhusiwa kutoka kwa shirika la chakula na dawa (TFDA) na vipo ambavyo vilipigwa marufuku kutokana na uwepo wa viambata sumu. Ni ngumu kuviweka hapa lkn kwa muda wako waweza kupita katika wavuti wa shirika la dawa na chakula tanzania kwa maelezo zaidi.

FAIDA YA VIPODOZI
Zipo faida nyingi za vipodozi kutokana kwamba vimetengenezwa kwa sababu  maalumu. Kubwa kabisa likiwa ni kuweka ngozi katika hali aidha ya unyevu au ukavu na kurutubisha ngozi. Pia, kipodozi kinakufanya kunukia na kuonekana vizuri mbele za watu. Vilevile baadhi ya vipodozi hutumika kama dawa.
MADHARA YA VIPODOZI VYENYE VIAMBATA SUMU
1.   Kipodozi chenye kiambata sumu kinaua wadudu ambao wanalinda ngozi (normal flora) hivyo kupunguza uwezo wa ngozi kulinda mwili. Kama tunavyojua kwamba ngozi  ni ogani ambayo moja ya kazi zake ni kulinda mwili kwa kuzuia wadudu kama bakteria na virusi kuingia ndani ya mwili na kuleta madhara. Hivyo basi unapotumia kipodozi ambacho kina kiambata sumu ni dhahiri kwamba unapunguza uwezo wa ngozi kulinda mwili.
2.   Viambata sumu vingine vinaweza kubadilisha mfumo wa kawaida wa mgawanyiko wa seli mwilini na kuufanya uwe isivyo kawaida. Hiyo inapelekea kuwa miongoni mwa hali hatarishi(risk factor) kwa magonjwa ya kansa ya ngozi
3.   Viambata sumu vingine vinaweza kuunguza ngozi moja kwa moja kwasababu vinaondoa tabaka la ngozi ambayo huzuia mionzi ya jua. Badala yake mionzi ya jua itapita moja kwa moja na kukuletea madhara mojawapo ikiwa ni kuungua.
BAADHI YA VIAMBATA SUMU VILIVYOAINISHWA NA TFDA
-         Bithionol
-         Hexachlorophene
-         Mercury compounds
-         Vinyl chloride
-         Zirconium
-         Steroids
-         Chloroform
-         Nk…..

No comments:

Post a Comment