Thursday, October 29, 2015

JIKINGE NA KIPINDUPINDU KAMA HIVI1.   Tumia maji safi na salama katika;

-         Kunywa

-         Kupigia mswaki

-         Kutengenezea barafu( kwa wale wafanya biashara au hata kwa matumizi ya nyumbani)

-         Osha vyombo vya kulia chakula kwa maji safi na salama. Tena vikauke kabla ya kutumia.

-         Safisha jikoni

2.   Osha mikono yako kwa maji safi na salama mara kwa mara.

3.   Tumia choo chako kwa usafi

4.   Pika chakula kiive vizuri…kifunikwe wakati wote….kula kikiwa cha moto…menya matunda na mboga za majani

Thursday, October 22, 2015

JE DALILI ZA UGONJWA WA KIFUA KIKUU (TB) NI ZIPI?

Kifua kikuu(TB )ni ugonjwa unaosababishwa na bacteria anaejulikana kwa jina la Mycobacterium tuberculosis.

Mycobacterium tuberculosis ni aina ya bacteria anaesababisha TB kwa binadamu….ingawa zipo jamii zingine za Mycobacterium zinazoweza pia kusababisha TB kwa binadamu. Bacteria huyu anaweza kuingia kwa binadamu na kusababisha TB  katika mfumo wowote wa binadamu. Mfano mtu anaweza kuwa na TB ya mapafu, figo, ktk mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, ktk ngozi, ubongo nk….

JINSI YA KUENEA

1.   Njia kuu ya kuenea ni kwa Kuvuta hewa yenye wadudu hao. Hii ni kutokana aidha na kuishi au kuwa karibu na mtu mwenye ugonjwa huo. Na mara anapopiga chafya au kukohoa bila kufunika mdomo ndipo wadudu hao wanaweza kukupata.

2.   Kula vyakula visivyopikwa vikaiva vizuri. Kuna jamii ya watu wanaokunywa maziwa ambayo hayajachemshwa pia wako ktk hatari ya kupata bacteria hao.

DALILI ZA UGONJWA WA KIFUA KIKUU(TB)

1.   Kikohozi cha muda mrefu

2.   Kukohoa damu

3.   Homa isiyoisha

4.   Kupungua uzito kusiko kawaida

5.   Na pia maumivu ya kifua wakati wa kukohoa.

6.   Dalili zingine ni kupungua hamu ya kula,kuchoka na kutoka jasho wakati wa usiku.

NAMNA YA KUZUIA

1.   Hakikisha unapokohoa  au kupiga chafya unafunika mdomo wako ili kuepuka kumuambukiza mwingine.

2.   Unapotema mate hakikisha unayafukia vizuri

3.   Unapoishi na mtu mwenye ugonjwa wa TB hakikisha unapata elimu ya namna ya kuishi nae bila kupata maambukizi ya ugonjwa huo

4.   Nenda hospitali mara unapokua na dalili zinazofanana na hizo hapo juu ili kujihakikishia afya yako.