Wednesday, September 16, 2015

KUTOA MIMBA (ABORTION)


 

Utoaji mimba au abortion kwa neno la kitaalamu, ni kitendo cha mwanamke mjamzito kukomesha mimba  kabla ya kufikia wiki 28 ya ujauzito aidha kwa sababu za kitaalamu au kinyume na sheria. Lakini kutokana na Shirika la Afya Duniani(WHO) linatoa maana ya abortion kama kitendo cha kukatisha mimba kabla ya ujauzito kufikia wiki 22.

AINA ZA ABORTION

1.   LEGAL ABORTION:  ni aina ya abortion inayofanywa kwa sababu za kiafya. Mfano kama kichanga kufia tumboni ni lazima kitolewe katika mazingira ya hospitalini ili kuokoa maisha ya mama. Hali hiyo ya mtoto kufia tumboni inasababishwa na mambo mengi mfano mama kupata ajali ambayo inaweza kumdhuru mtoto tumboni,mama kupata magonjwa mbalimbali wakati wa ujauzito kama vile magonjwa ya zinaa nk. Ili kuhakikisha kwamba ni abortion lazima uende kwa daktari ili akuhakikishie kitaalamu baada ya kuona dalili za hatari kwa mama mjamzito.

2.   ILLEGAL ABORTION: ni kitendo cha kukomesha ujauzito kinyume na sheria. Vijana wengi wa kike walioko na wasiokua kwenye ndoa wanatoa mimba kinyume na sheria kwa sababu wanazozijua wenyewe, kitendo ambacho ni hatari na hufanywa katika mazingira ya mafichoni na yasiyokua salama kutokana na vifaa wanavyotumia ambavyo haviko salama.

-         Kutokana na takwimu za Shirika la Afya Duniani zinaonyesha kwamba asilimia 50% ya vifo vya mama wajawazito zinatokana na abortion.hiyo inamaanisha katika vifo viwili vya mama wajawazito, mmoja ni kwasababu ya abortion.

HATARI ZA KUTOA MIMBA (ILLEGAL ABORTION)

1.   Kutokwa damu nyingi:  kitendo cha kutoa mimba ni hatari kwasababu  mama anapoteza damu nyingi sana, hali ambayo inaweza kumpelekea kupata shock na hatimaye kufariki. Kumbuka mimba inapotungwa mishipa ya damu ya mtoto huundwa ili kutengeneza mawasiliano kati ya mama na mtoto hivyo inapochokonolewa hupasuka na kumwaga damu nyingi hali ambayo ni hatari sana kwa mama.

2.   Kupata maambukizi ya bacteria kwenye damu: kwa watu wanaofanya abortion mara nyingi vifaa wanavyotumia pamoja na mazingira wanapofanyia sio salama hali ambayo inapelekea wadudu kuingia katika mji wa uzazi na kusababisha maambukizi  na kusababisha maambukizi kwenye damu.

3.   Wakati wa abortion, kutokana na vifaa vinavyotumika  na namna inavyofanyika, inaweza pia kusababisha baadhi ya viungo vilivyo karibu na mji wa uzazi pia kuharibiwa mfano, kibofu na utumbo hali ambayo ni hatari sana.

4.   Wakati mwingine kama imeshatokea mama kafanya abortion na anatokwa na damu nyingi sana pamoja na kuishiwa nguvu, akipelekwa hospitalini huongezewa damu jambo ambalo pia linaweza kumuweka katika hatari ya kupata baadhi ya magonjwa ya kuambukiza kupitia damu kama homa ya ini.

5.   Mwanamke ambaye anafanya abortion yuko katika hatari ya kupata abortion kwa ujauzito ujao kwasababu tayari mji wa uzazi umekosa (miundombinu) ya kuweza kuhifadhi na kutunza mtoto.

6.   UTASA: kutokana na tafiti zilizofanywa pia zinaonyesha kwamba kutoa mimba sana kunachangia mabadiliko ya vichochezi (hormones) za mwanamke hivyo kuleta tatizo la utasa.

UHALISIA:

-         Kiuhalisia na kimaadili, hakuna dini inayoruhusu kutoa mimba, hivyo jamii inapaswa kuelimishana kuhusu kuacha kufanya kitendo hiki ambacho ni uuaji na ukatili. Kumbuka maisha ya mtoto yanaanza pale tu mimba inapotungwa, hivyo kutoa mimba ni kuua mtoto asiyekua na hatia, ni dhambi……. Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wameshawahi kutoa au unafikiria kutoa tafadhali acha, fikiri tofauti, lea mtoto, ni kiumbe cha Mungu kama wewe!

-         ELIMISHA NA WENGINE…..ASANTE KWA KUSOMA.

 

“LIKE” UKURASA WETU WA FACEBOOK (BWAMBO HEALTH FARM) ILI KUPATA UPDATES

KWA USHAURI ,MAONI AU MASWALI TUANDIKIE- agripambwamboo@gmail.com

0716648735/0688648735

 

 

 

No comments:

Post a Comment