Saturday, December 5, 2015

DALILI ZA KIPINDUPINDU


 

  Kuharisha  mfululizo au mara kwa mara bila tumbo kuuma ambako kunaweza kuambatana na kutapika

  Kinyesi au matapishi huwa ya majimaji yasiyo na harufu, yanayofanana na maji yaliyooshewa mchele

  Kusikia kiu sana, macho kudidimia na ngozi kusinyaa ambavyo hutokana na upungufu wa maji mwilini

  Kuishiwa nguvu,kuhema haraka haraka na kulegea. Hali hii hutokana na upungufu wa maji na madini mwilini.

Monday, November 9, 2015

ATHARI ZA KUTOTUMIA DAWA KAMA ILIVYOELEKEZWA NA DAKTARI/MTAALAMU WA AFYA.


Tokeo la picha la drugs imageTokeo la picha la drugs imageTafiti mbalimbali zimeonyesha kwamba watu wengi hawatumii dawa (dozi) kama inavyotakiwa. Hii ni kutokana na sababu zifuatazo:

-      Kupata nafuu ya ugonjwa kabla ya kumaliza dawa alizoandikiwa na daktari.

-      Umri: wazee na watoto kwa kawaida walio wengi hawapendi kutumia dawa hivyo kutomaliza dozi.

-      Kutokujua kusoma, kuandika na kuhesabu

-      Kutopata elimu ya kutosha ya afya

-      Umaskini; wagonjwa wengine kutokana na hali zao za kiuchumi kushindwa kununua kiasi cha chawa alichoandikiwa na daktari

-      Kwa nia ya kutaka kujiua. Baadhi ya watu wanajiongezea  kiasi walichoandikiwa na daktari/mtaalamu wa afya kwa lengo la aidha kutaka kujiua.

-      Nk.

 
ATHARI ZA KUTOMALIZA DAWA(DOZI)

-      Kuujengea mwili usugu wa dawa iliyotumika na dawa zingine zenye ufanano. Hii hutokana na ukweli kwamba unatumia dawa ili kuua vimelea vinavyosababisha ugonjwa husika au kuvimaliza nguvu. Ikiwa utatumia chini ya kiasi au zaidi ya kiasi ulichoandikiwa na daktari/ mtaalamu wa afya, vimelea vya ugonjwa husika vinajitengenezea usugu wa dawa hiyo ambapo ukija kutumia dawa hiyo tena inakua haifanyi kazi ipasavyo. Ndiyo maana wakati mwingine mtu anakua na ugonjwa usioisha (sugu), ambapo angekua anatumia kama ilivyoagizwa angepona.

-      Dawa isipotumika vizuri kama

WHY SMOKING WHEN YOU DRINK ALCOHOL


According to the Medical Daily Reports, scientists have discovered the reason  why people  become social smokers while drinking alcohol. Researchers at the University of Missouri believe that people crave the effects of nicotine- (which is a chemical found in cigarettes), when drinking as it helps to offset the feelings of sleepiness induced by alcohol.

Remember: cigarette smoking is dangerous for your health as it causes many health problems, more of cardiac and cancer. Take precaution, stop smoking .
Tokeo la picha la cigaretteTokeo la picha la cigarette           

Thursday, October 29, 2015

JIKINGE NA KIPINDUPINDU KAMA HIVI1.   Tumia maji safi na salama katika;

-         Kunywa

-         Kupigia mswaki

-         Kutengenezea barafu( kwa wale wafanya biashara au hata kwa matumizi ya nyumbani)

-         Osha vyombo vya kulia chakula kwa maji safi na salama. Tena vikauke kabla ya kutumia.

-         Safisha jikoni

2.   Osha mikono yako kwa maji safi na salama mara kwa mara.

3.   Tumia choo chako kwa usafi

4.   Pika chakula kiive vizuri…kifunikwe wakati wote….kula kikiwa cha moto…menya matunda na mboga za majani

Thursday, October 22, 2015

JE DALILI ZA UGONJWA WA KIFUA KIKUU (TB) NI ZIPI?

Kifua kikuu(TB )ni ugonjwa unaosababishwa na bacteria anaejulikana kwa jina la Mycobacterium tuberculosis.

Mycobacterium tuberculosis ni aina ya bacteria anaesababisha TB kwa binadamu….ingawa zipo jamii zingine za Mycobacterium zinazoweza pia kusababisha TB kwa binadamu. Bacteria huyu anaweza kuingia kwa binadamu na kusababisha TB  katika mfumo wowote wa binadamu. Mfano mtu anaweza kuwa na TB ya mapafu, figo, ktk mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, ktk ngozi, ubongo nk….

JINSI YA KUENEA

1.   Njia kuu ya kuenea ni kwa Kuvuta hewa yenye wadudu hao. Hii ni kutokana aidha na kuishi au kuwa karibu na mtu mwenye ugonjwa huo. Na mara anapopiga chafya au kukohoa bila kufunika mdomo ndipo wadudu hao wanaweza kukupata.

2.   Kula vyakula visivyopikwa vikaiva vizuri. Kuna jamii ya watu wanaokunywa maziwa ambayo hayajachemshwa pia wako ktk hatari ya kupata bacteria hao.

DALILI ZA UGONJWA WA KIFUA KIKUU(TB)

1.   Kikohozi cha muda mrefu

2.   Kukohoa damu

3.   Homa isiyoisha

4.   Kupungua uzito kusiko kawaida

5.   Na pia maumivu ya kifua wakati wa kukohoa.

6.   Dalili zingine ni kupungua hamu ya kula,kuchoka na kutoka jasho wakati wa usiku.

NAMNA YA KUZUIA

1.   Hakikisha unapokohoa  au kupiga chafya unafunika mdomo wako ili kuepuka kumuambukiza mwingine.

2.   Unapotema mate hakikisha unayafukia vizuri

3.   Unapoishi na mtu mwenye ugonjwa wa TB hakikisha unapata elimu ya namna ya kuishi nae bila kupata maambukizi ya ugonjwa huo

4.   Nenda hospitali mara unapokua na dalili zinazofanana na hizo hapo juu ili kujihakikishia afya yako.

Wednesday, September 16, 2015

KUTOA MIMBA (ABORTION)


 

Utoaji mimba au abortion kwa neno la kitaalamu, ni kitendo cha mwanamke mjamzito kukomesha mimba  kabla ya kufikia wiki 28 ya ujauzito aidha kwa sababu za kitaalamu au kinyume na sheria. Lakini kutokana na Shirika la Afya Duniani(WHO) linatoa maana ya abortion kama kitendo cha kukatisha mimba kabla ya ujauzito kufikia wiki 22.

AINA ZA ABORTION

1.   LEGAL ABORTION:  ni aina ya abortion inayofanywa kwa sababu za kiafya. Mfano kama kichanga kufia tumboni ni lazima kitolewe katika mazingira ya hospitalini ili kuokoa maisha ya mama. Hali hiyo ya mtoto kufia tumboni inasababishwa na mambo mengi mfano mama kupata ajali ambayo inaweza kumdhuru mtoto tumboni,mama kupata magonjwa mbalimbali wakati wa ujauzito kama vile magonjwa ya zinaa nk. Ili kuhakikisha kwamba ni abortion lazima uende kwa daktari ili akuhakikishie kitaalamu baada ya kuona dalili za hatari kwa mama mjamzito.

2.   ILLEGAL ABORTION: ni kitendo cha kukomesha ujauzito kinyume na sheria. Vijana wengi wa kike walioko na wasiokua kwenye ndoa wanatoa mimba kinyume na sheria kwa sababu wanazozijua wenyewe, kitendo ambacho ni hatari na hufanywa katika mazingira ya mafichoni na yasiyokua salama kutokana na vifaa wanavyotumia ambavyo haviko salama.

-         Kutokana na takwimu za Shirika la Afya Duniani zinaonyesha kwamba asilimia 50% ya vifo vya mama wajawazito zinatokana na abortion.hiyo inamaanisha katika vifo viwili vya mama wajawazito, mmoja ni kwasababu ya abortion.

HATARI ZA KUTOA MIMBA (ILLEGAL ABORTION)

1.   Kutokwa damu nyingi:  kitendo cha kutoa mimba ni hatari kwasababu  mama anapoteza damu nyingi sana, hali ambayo inaweza kumpelekea kupata shock na hatimaye kufariki. Kumbuka mimba inapotungwa mishipa ya damu ya mtoto huundwa ili kutengeneza mawasiliano kati ya mama na mtoto hivyo inapochokonolewa hupasuka na kumwaga damu nyingi hali ambayo ni hatari sana kwa mama.

2.   Kupata maambukizi ya bacteria kwenye damu: kwa watu wanaofanya abortion mara nyingi vifaa wanavyotumia pamoja na mazingira wanapofanyia sio salama hali ambayo inapelekea wadudu kuingia katika mji wa uzazi na kusababisha maambukizi  na kusababisha maambukizi kwenye damu.

3.   Wakati wa abortion, kutokana na vifaa vinavyotumika  na namna inavyofanyika, inaweza pia kusababisha baadhi ya viungo vilivyo karibu na mji wa uzazi pia kuharibiwa mfano, kibofu na utumbo hali ambayo ni hatari sana.

4.   Wakati mwingine kama imeshatokea mama kafanya abortion na anatokwa na damu nyingi sana pamoja na kuishiwa nguvu, akipelekwa hospitalini huongezewa damu jambo ambalo pia linaweza kumuweka katika hatari ya kupata baadhi ya magonjwa ya kuambukiza kupitia damu kama homa ya ini.

5.   Mwanamke ambaye anafanya abortion yuko katika hatari ya kupata abortion kwa ujauzito ujao kwasababu tayari mji wa uzazi umekosa (miundombinu) ya kuweza kuhifadhi na kutunza mtoto.

6.   UTASA: kutokana na tafiti zilizofanywa pia zinaonyesha kwamba kutoa mimba sana kunachangia mabadiliko ya vichochezi (hormones) za mwanamke hivyo kuleta tatizo la utasa.

UHALISIA:

-         Kiuhalisia na kimaadili, hakuna dini inayoruhusu kutoa mimba, hivyo jamii inapaswa kuelimishana kuhusu kuacha kufanya kitendo hiki ambacho ni uuaji na ukatili. Kumbuka maisha ya mtoto yanaanza pale tu mimba inapotungwa, hivyo kutoa mimba ni kuua mtoto asiyekua na hatia, ni dhambi……. Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wameshawahi kutoa au unafikiria kutoa tafadhali acha, fikiri tofauti, lea mtoto, ni kiumbe cha Mungu kama wewe!

Friday, June 19, 2015

ELIMU JUU YA TETENASI( TETANUS)

Opisthotonus in a patient suffering from tetanus - Painting by Sir Charles Bell - 1809.jpg 
Tetenasi  ni ugonjwa unaosababishwa na bacteria wanaoitwa ( Clostridium tetani). Wadudu hawa wanapatikana katika mazingira yanayotuzunguka mfano; ardhi,misumaru au vitu vyenye ncha, vinyesi vya baadhi ya wanyama nk.

Bacteria wa tetenasi wanaweza kuishi katika mazingira kwa miaka mingi . Pia wanapenda vidonda, ndio maana wanaingia mwilini kupitia vidonda au mikwaruzo. Dalili za Tetenasi zinatokea siku 4-14 baada ya kupata jeraha.

Tetenasi imegawanyika sehemu mbili:

1.   Tetenasi inayotokea kwa watu wazima (adult)

2.   Tetenasi ya watoto (neonates)

 

NANI YUPO HATARINI KUPATA TETENASI?

KWA WATU WAZIMA(ADULTS)

1.   Ikiwa umeumia na kupata jeraha  au kidonda sehemu ya mwili wako uko katika hatari ya kupata ugonjwa huu hatari wa tetenasi.

2.   Ikiwa umetobolewa na msumari una zaidi ya 32% kupata tetenasi

3.   Ikiwa umeungua, au watu wanaojidunga sindano za madawa ya kulevya,  au watu wanaojiwekea tattoo, watu wenye magonjwa ya meno, wapo katika hatari ya kupata ugonjwa huu

4.   Kisukari ni moja ya hali inayoweza kukusababishia tetenasi

5.   Pia upasuaji (surgery) isiyo salama, mfano matumizi ya vyombo visivyo salama(unsterilized)

KWA WATOTO

1.   Kama mama mjamzito hatapata chanjo ya tetenasi , au kujifungulia nyumbani, yupo kwenye hatari ya kumsababishia mtoto mchanga kupata tetenasi.

DALILI ZA TETENASI

1.   Kukakamaa kwa misuli, mdomo kushindwa kufunguka(lock-jaw)

2.   Kutokwa na jasho jingi, homa kali

3.   Kushindwa kumeza kwasababu ya kukakamaa kwa misuli.

4.   Kutokwa na udenda(drooling)

5.   Kupata matatizo ya kupumua.

KINGA;

-         Tafadhali nenda hospitalini au kituo cha afya mara baada ya kupata jeraha lolote ili kupata chanjo ya tetenasi

-         Kwa wafanyakazi wa afya, ni muhimu kupata chanjo ya tetenasi kwasababu ya mazingira hatarishi  ya kazi.

-         Kwa mama mjamzito tafadhali hakikisha unapata chanjo zote za tetenasi  ili kujikinga na pia kumkinga mtoto. Pia unapoona dalili za uchungu hakikisha unawahi ukajifungulie kituo cha afya mapema.

-         Epuka majeraha yasiyokua ya lazima, vaa viatu, weka vitu vyenye ncha kali mbali na watoto.

-         Mpeleke mtoto atahiriwe hospitalini na sio kwa mtaani, kwasababu ya hatari kubwa iliyopo ya kupata tetenasi.