Monday, December 15, 2014

TATIZO LA KUFIKA KILELENI MAPEMA (PREMATURE EJACULATION)


 

Premature ejaculation ni hali isiyokua ya kawaida ya mwanaume kufika kileleni ndani ya dakika moja mpaka mbili wakati wa kujamiiana na wengine kuchukua nusu dakika au hata robo dakika,na tatizo hilo liwe na muda kuanzia miezi sita na kuendelea toka lianze. Tatizo hili limekua likiwapata watu wengi wakiwemo vijana. Kutokana na utafiti uliofanyika umeonyesha kwamba 20%-30% ya  wanaume kuanzia miaka 18-70 wanapata premature ejaculation.

-         Tatizo hili linaweza kuwa limeanza tu mara baada ya kupevuka au,

-         Limeanza baada ya kukaa muda mrefu baada ya kupevuka (late onset).

KWANINI PREMATURE EJACULATION?

-         Sababu zinazotokana na wawili hao( partner factors) mfano,hali za kiafya za wawili hao.

-         Sababu za kimahusiano(relationship factors) mfano,mawasiliano duni(poor communications),utofauti wa utayari wa kujamiiana.

-         Sababu binafsi mfano,mtu aliyewahi kujeruhiwa kimapenzi,msongo wa mawazo,kufukuzwa kazi nk.

-         Tatizo hili pia linaweza kuwa la kurithi

-         Poa wanaume ambao  wana matatizo ya kisaikolojia.

MATOKEO YAKE;

-         Kwanza mwanaume anashindwa kujiamini (poor self esteem)

-         Kuvunjika kwa mahusiano/ndoa.

-         Msongo wa mawazo(stress)

-         Pia hili tatizo linaweza kuhusianishwa na kukosa uwezo wa kumpa mwanamke mimba(conceive), japo ni kwa asilimia ndogo sana.

NB.. unapoona una hilo tatizo tafadhali nenda kamuone daktari kwenye hospitali iliyo karibu nawe.usione aibu!

Kama una swali,ushauri piga

 +255 716648735 au +255 688648735


Tembelea ukurasa wetu wa facebook na gonga like kwa updates…….  Andika’ bwambo health farm’

No comments:

Post a Comment