Wednesday, September 17, 2014

MTAZAMO KUHUSU UKEKETAJI


 

Ukeketaji ni utamaduni wa kuondoa sehemu ya nje ya sehemu ya uke. Kiuhalisia ukeketaji unafanywa na mangariba, na hutumia vifaa kama nyembe,visu,glass,mikasi, mawe yaliyochongoka na kucha ndefu ,aidha kwa ganzi ama laa!. Hii ilianza miaka ya zamani pale jamii ilipokua ikifanya vitendo hivyo kwa malengo yao binafsi kutokana na jamii husika kutokana na mila na desturi zao.

Umri ambao mschana hufanyiwa ukeketaji ulikua ni kuanzia miaka 5 hadi 14. Ndipo shirika la afya duniani WHO na shirika la mfuko wa watoto la kimataifa UNICEF liliingilia kati na kuanza kutoa elimu juu ya madhara yanayomkuta mtoto anapofanyiwa tohara hiyo, kwa kuonyesha madhara yake kiafya  na pia kulichukulia swala hilo kama ni unyanyasaji usiokua wa lazima, kwani faida zake ni chache ukilinganisha na adha anayoipata mtoto.

Yapo madhara anayoyapata mtoto mara baada ya kufanyiwa ukeketaji (acute complications) na pia yapo madhara anayopata mtoto ya kudumu ( chronic complications).

MADHARA KIAFYA;

-         Kutokwa na damu hadi kufa

-         Kushindwa kukojoa kawaida ( urinary retention)

-         Magonjwa ya njia ya mkojo

-         Bacteria kuingia sehemu ya kidonda na kuathiri mfumo mzima wa damu (septicemia)

-         Pia wanapata tetenasi kutokana na kutumia vifaa visivyokua visafi (sterile)

-         Wanapata pia ugonjwa wa homa ya ini, na HIV

-         Wanapata maumivu makali sana wakati wa kujamiiana

-         Wanapata magonjwa ya mfumo wa uzazi

-         Wakati wa kuzaa wanaweza kupata matatizo ya fistula

-         Asilimia kubwa ya wanawake waliokeketwa huwa wanachanika sana wakati wa kuzaa

-         NK

WAKE UP!!!!

Jamii lazima ipinge swala hili la ukeketaji vikali ili kunusuru watoto kwenye adha isiyokua ya lazima na kutotumia mila kuwakandamiza watoto.

Monday, September 15, 2014

DAKTARI AELEZA MADHARA YA KUJICHUBUA

 
Kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanyika imeonekana kuwa kujichubua kulianza zamani lakini karne ya 19 ndio hali hiyo ilianza kuonekana zaidi, huku watu wengi wakiamini kujichubua ndio wanakua na mvuto zaidi, kitu ambacho sio kweli kwasababu Mungu alimuumba kila mtu kwa mfano wake. Na hakuna mtu mzuri na mbaya kwa sura.
Wakati hali hiyo ikiendelea, watu wengi wameonekana  kuwa na magonjwa hasa ya ngozi ambayo mengi hayatibiki.
-         Kutokana na kujichubua watu hupata kansa ya ngozi kwasababu kemikali zinazotumika kujichubua zinaondoa melanin ambayo ipo  katika ngozi ambayo ni muhimu kwa kutoa ulinzi wa ngozi dhidi ya miale ya jua ambapo kwa kujichubua,  mionzi hiyo hupenya na kuua seli zinazozalisha  melanin hatimaye kubadilisha mfumo wa kuzaliana kwa seli za ngozi na kusababisha kansa ya ngozi.
-         Mtu anayejichubua huungua sana  sana wakati wa jua au kukaa karibu na moto
-         Kisaikolojia mtu anayejichubua hayuko sawa, lazima kuna jambo lililomfanya kuamua kujichubua 
KUMBUKA; kujichubua sio urembo ama utanashati,,,kwanza lazima ujikubali jinsi ulivyoumbwa na Mungu, kuwa msafi na ujipende,usiige,be yourself…….