Thursday, August 14, 2014

UMUHIMU WA KLINIKI KWA MAMA MJAMZITO


 

Kwa kawaida mama mjamzito anaanza kliniki na anatakiwa kuhudhuria mara nne kama hana matatizo yoyote. Hii ni kutokana na utaratibu uliowekwa na wizara ya afya na ustawi wa jamii. Wizara imeweka mambo ambayo mama mja mzito atatakiwa kupewa kama haki yake ikiwa na lengo kuu la kupunguza vifo vya mama na mtoto ambavyo hapo awali vilikua vingi sana.

Katika kutoa huduma hiyo ambayo ipo hata katika zahanati, kuna mambo ya msingi ambayo mama atapewa.

HUDUMA GANI ANATAKIWA KUPEWA????

1.  Huduma kama;kupima uzito,kupima presha,kupima wingi wa damu,kupima kama mtoto anacheza tumboni.

2.  Kumpatia mama vidonge vya kuongeza damu(folic asidi na feras sulfeti)

3.  Kupewa vidonge vya SP ili kumkinga na malaria

4.  Vidonge vya minyoo

5.  Sindano ya pepopunda

6.  Pia mama anatakiwa apewe ushauri kuhusu dalili za hatari,uzazi wa mpango,maandalizi ya kujifungua,magonjwa yatokanayo na kujamiiana na matumizi sahihi ya kondomu

7.  Pia anatakiwa kupimwa VVU,kaswende,grupu la damu

8.  Pia atapimwa tumbo

ATHARI YA KUTOPATA HUDUMA HIZO

Mama mjamzito asipopatiwa huduma hizo ana hatari ya;

-         Anaweza kupata matatizo ya presha( kifafa cha mimba)

-         Matatizo wakati wa kuzaa ambayo yanaweza kumpelekea mtoto kufa

-         Mtoto anaweza kuzaliwa njiti

-         Mtoto anaweza kuzaliwa akiwa na magonjwa mbalimbali

-         Pia mama anaweza kupoteza uhai wake.

KUMBUKA KATIKA MAMBO AMBAYO YANACHANGIA VIFO VYA MAMA WAJAWAZITO NA WATOTO NI KUKOSA HUDUMA THABITI ZA AFYA.

 

IMEANDALIWA NA;  BWAMBO HEALTH FARM TEAM

KWA USHAURI,SWALI AU MAONI; +255716648735  AU  +255688648735

Kama hujaLIKE page yetu ya facebook tafadhali LIKE ili upate taarifa muhimu kwa afya yako.

No comments:

Post a Comment