Saturday, August 23, 2014

TAMBUA MATUMIZI SAHIHI YA KONDOM

the hand of a young woman pulling a condom to prevent pregnancy from her jeans pocket - stock photocondom - stock photoCondom use icons - stock vector
 

Awali ya yote jamii inabidi ifahamu ukweli kuhusu matumizi sahihi ya kondomu kwasababu ninaamini watu wengi wanafikiri wapo katika njia sahihi ya kujikinga na maradhi mbalimbali kwa kutumia kondomu lakini badala yake wanakosea kutumia ipasavyo,hivyo kupata maambukizi ya maradhi hayo. Au unaweza kukosea kuitumia ukasababisha mwanamke kupata mimba, jambo ambalo halikua lengo lenu.

HATUA ZA KUTUMIA KONDOMU YA KIUME

-         Kwanza, kabla ya kununua angalia tarehe kama imeshaexpire au la! Pia kama kasha lake limetoboka. Usinunue!

-         Baada ya kununua ifungue taratibu kwasababu,kwa kadri unavyoivuta sana ndivyo inaweza kuchanika kwa wepesi

-         Ifungue kama ilivyoelekezwa katika pakiti yake

-         Wakati wa kuivaa shikilia sehemu ya mwisho (tip) na uache nafasi katika (tip) ya kondomu ambayo iko kwa ajili ya kushikilia shahawa wakati wa kujamiiana

-         Vaa kondomu kwenye uume uliosimama(erect penis)

-         Kama umekosea kuivaa, usivae tena bali uvue na kuitupa,kasha uchukue nyingine

-         Baada ya kujamiiana vua kondomu kwa kuvuta kutoka mwisho(tip) wakati bado uume ukiwa umesimama (erect)

-         Tumia kondomu nyingine kama unataka kuendelea

NB; wengine wanaamini kuvaa kondomu mbili au zaidi ndo inazuia maambukizi! La hasha! Vaa kondomu moja tu.

Na kumbuka kuwa matumizi ya kondomu hayazuii maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa asilimia 100.

Kwahiyo ;

1.  Epuka kufanya ngono zembe

2.  Kuwa mwaminifu na mpenzi mmoja uliye naye

 

IMEANDALIWA NA; BWAMBO HEALTH TEAM

KWA SWALI,USHAURI AU MAONI; email us, agripambwamboo@gmail.com

NAMBARI  +255 716648735  AU  +255 688648735

Kama hujaLIKE katika ukurasa wetu wa facebook,tafadhali fanya hima na alike marafiki zako ili nao waLIKE ili wapate elimu ya afya ambayo ni haki ya kila raia Duniani.

 -Bwambo Health Farm tupo kwa ajili yako,kwa afya yako…………………

 

No comments:

Post a Comment