Tuesday, August 12, 2014

SOMA: UMUHIMU WA MAMA KUMNYONYESHA MWANAE


 

Mashirika ya afya pamoja na tafiti mbalimbali zilizofanyika duniani zimebainisha kwa kina sana juu ya umuhimu wa mama kumnyonyesha mtoto. Hii ni kwasababu, kutokana na utandawazi, kina mama wengi kutokana na majukumu ya kikazi hawanyonyeshi watoto wao, huku wakiwanywesha maziwa ya wanyama mfano ng’ombe au mbuzi.

Lakini na ijulikane kuwa maziwa ya mama yana virutubisho tofauti kabisa na ya ng’ombe au mbuzi, ya mama ni kwa ajili ya mtoto na ya ng’ombe ni kwa ajili ya ndama.

JE KUNA FAIDA GANI YA KUNYONYESHA?

1.  Yana kinga ya mwili kwa mtoto dhidi ya bacteria na virus wanaosababisha mtoto kuharisha,homa ya mapafu(pneumonia),homa ya uti wa mgongo

2.  Maziwa ya mama yana virutubisho vyote muhimu vinavyomjenga mtoto kiukuaji,yaani,protini,carbohydrate,mafuta,vitamin,madini,na maji.

3.  Pia ukimnyonyesha mtoto wako unamjenga kisaikolojia,tafiti nyingi zimetanabaisha tofauti ya watoto walionyonyeshwa na ambao hawakunyonya.

4.  Maziwa ya mama yana joto ambalo linahitajika kwa mtoto

5.  Maziwa ya mama hayana contamination ya bacteria hasa akinyonyesha kwa usafi

6.  Nk.

 

Ref.Nelson tx book of paediatrics

IMEANDALIWA NA; BWAMBO HEALTH FARM

KWA USHAURI,SWALI AU MAONI: +25516648735 AU +255688648735

Tembelea face book page yetu na like kwa updates

 

 

No comments:

Post a Comment