Thursday, August 21, 2014

MAMBO AMBAYO MAMA MJAMZITO ANATAKIWA KUWA MAKINI ANAPOYAONA

 
Mama mjamzito ni haki yake kupendwa na kulindwa kwasababu amebeba mtoto tumboni ambaye ni faidal kubwa sana katika jamii. Hivyo basi, ni lazima jamii sasa ibadilike na kuona umuhimu wa kwenda kucheki afya zao mara kwa mara hospitalini.
Kwa mama mjamzito,kuna baadhi ya mambo ambayo pindi anapoyaona asisubiri hata lisaa nyumbani,badala yake aende hospitalini haraka iwezekanavyo ili apate huduma kutoka kwa daktari na wahudumu wa afya sehemu husika.
MAMBO HAYO NI:
-         Kutokwa na damu sehemu za siri (vaginal bleeding)
-         Kutokwa na maji yanayotokana na kupasuka kwa chupa (vaginal discharge)
-         Kuwa na homa kali(kuchemka)
-         Kuwa na uchungu  kwa mimba yenye umri wa wiki 34
-         Kupungua kucheza kwa mtoto au kutocheza kabisa
-         Miguu kuvimba
-         Kichwa kuuma sana
-         Pia anapokuwa amefika hospitalini ,kama amepimwa pressure na ikawa zaidi ya 140/90 na zaidi,hiyo pia ni hali ya hatari
-         Kama pia mama amerukwa na akili wakati wa ujauzito afike hospitalini haraka iwezekanavyo
NB; KUMBUKA! Lengo ni ili kila Mtanzania na dunia nzima waelewe kuhusu umuhimu wa kwenda hospitalini
IMEANDALIWA NA ; BWAMBO HEALTH FARM TEAM
KWA USHAURI,SWALI,MAONI WASILIANA KUPITIA; agripambwamboo@gmail.com
NAMBARI; +255 716648735  AU +255 688648735
LIKE ukurasa wetu wa facebook kwa shule zaidi
☺♥ Bwambo Health Farm tupo kukupa shule ya ukweli………………

No comments:

Post a Comment