Tuesday, August 12, 2014

JE MAMA MWENYE VIRUSI VYA UKIMWI ANARUHUSIWA KUNYONYESHA?


 
Kwa kawaida mama anatakiwa kumnyonyesha mtoto kwa takribani mwaka mmoja hadi miaka miwili na kuendelea. Na katika miezi sita ya mwanzoni mama ni lazima amnyonyeshe mwanae bila kumpa kitu kingine chochote,hata maji ya kunywa hayaruhusiwi! Ndipo baada ya miezi sita mama anaruhusiwa kumuanzishia mtoto vyakula vingine kama uji wa lishe,maji nk.

Na ikumbukwe kuwa unapomuanzishia mtoto kitu kingine tofauti na maziwa ya mama katika miezi sita ya mwanzo,unamuweka mtoto kwenye mazingira ya kupata maambukizi ya bacteria na virus kutokana na umuhimu wa maziwa ya mama. Hii ni kutokana na tafiti zilizofanya na shirika la afya duniani (        WHO).

JE KWA MAMA ALIYEATHIRIKA???

Kwa mama mwenye virusi vya ukimwi anashauriwa kunyonyesha mtoto wake hadi mwaka mmoja tu,zaidi ya hapo mtoto ana hatari ya kupata maambukizi kwasababu ya ule msuguano wa mtoto anaponyonya. Atafuata utaratibu wa kawaida wa kunyonya tu kwa miezi sita ya mwanzo alafu hii mingine atamchanganyia kama kawaida kwa mwaka mmoja tu ndipo ataacha kumnyonyesha.

BWAMBO HEALTH FARM TUNAJALI AFYA YAKO

 

KWA MASWALI,USHAURI,MAONI; +255716648735   AU +255688648735


Kwa updates zaidi tembelea ukurasa wetu wa facebook na like.

No comments:

Post a Comment