Wednesday, August 20, 2014

ELIMU KUHUSU UGONJWA WA EBOLA


 

Virusi vya ebola viligunduliwa hapo awali mwaka 1976 katika jamhuri ya kidemocrasia ya Congo ( Zaire) na Sudan. Ugonjwa wa ebola ulipewa jina hilo baada ya kugunduliwa huko Congo  kutokana na mto unaoitwa (Ebola river)  huko Congo.

Ugonjwa huu wa ebola unasababishwa na virusi vinavyojulikana kwa jina la Ebolavirus.

Ugonjwa huu unaenezwa kwa njia zifuatazo;

1.  Mgusano wa damu au utepetepe (body fluids) kutoka kwa mtu aliye na virusi vya ebola

2.  Mgusano wa vifaa vya hospitalini hasa sindano zilizohudumia mtu mwenye virusi hivyo pia vinaweza kusambaza ugonjwa huo

3.  Shahawa kwa mtu mwenye ebola pia zimeripotiwa kusambaza virusi hivyo vya ebola

4.  Pia mtu aliyefariki kwa ugonjwa wa ebola anaweza kupata virusi hivyo kama atagusa maiti hiyo bila kuvaa vifaa vya kujikinga.

5.  Shida pia ni kwa wahudumu wa afya ambao wanahudumia maelfu ya watu bila kujua yupi ni yupi mwenye ugonjwa huo bila kuvaa vifaa maalumu vya kujikinga

NB; Njia ya hewa haijagundulika kama inaweza kusambaza virusi hivyo,lakini  uchunguzi bado unaendelea .

DALILI ZA UGONJWA WA EBOLA

-         Katika hatua ya awali ya ugonjwa wa ebola, mgonjwa anakua na mafua yanayoambatana na uchovu,homa,kichwa kuuma,kuuma kwa viungo vya mwili,misuli na tumbo.

-         Kichefuchefu,kutapika damu, kuharisha damu ,na kuishiwa hamu ya kula

-         Dalili zingine kama,koo kukauka,kifua kuuma,kwikwi,kupata shida wakati wa kumeza na kupumua.

-         Pia mgonjwa anaweza kuota viupele mwilini.

NB; Tangu mtu aambukizwe virusi hivyo mpaka atakapoonyesha dalili,huwa inachukua siku 8 hadi 10.

TIBA;

Mpaka sasa hakuna dawa madhubuti ya kutibu ugonjwa huu wa ebola. Ila tu mgonjwa anapewa dawa zinazopunguza makali ya hizo dalili anazokua nazo.

 

IMEANDALIWA NA: BWAMBO HEALTH TEAM

KWA SWALI, USHAURI NA MAONI: agripambwamboo@gmail.com

MAWASILIANO: +255 716648735  AU  +255 688648735

Kama bado hujaLIKE ukurasa wetu wa facebook, LIKE ili upate habari nzuri za kiafya zenye kukujenga, na ni haki ya kila mtu kuipata.

No comments:

Post a Comment