Sunday, August 31, 2014

FAHAMU MADHARA YA MIRUNGI(GOMBA,MIRAA) KIAFYA


 

HISTORIA;

Ni mmea ambao una majina mengi kulingana na eneo,mfano gomba,miraa,mirungi nk.

Shirika la afya duniani WHO limetangaza kuwa zaidi ya masaa 14.6 milioni yanapotezwa kila siku kwa ulaji wa mirungi huko Yemen. Ulaji wa mirungi ulianzia Ethiopia,ukaenea hadi nchi za Afrika Mashariki,Yemen,Zimbabwe,Zambia,Malawi na hata Afrika kusini.

Mirungi ilionekana kuwa ni moja ya madawa ya kulevya hivyo ikakatangazwa na umoja wa mataifa UN na kupigwa marufuku mwaka 1971 kwasababu ya ufanano wa kemikali iitwayo amphetamine.

Yapo madhara mengi ya kiuchumi, kidini nk. Lakini yafuatayo ni madhara ya kiafya ya mirungi kama ilivyofanywa na shirika la afya duniani kama ifuatavyo;

MADHARA YA KIAFYA;

-         Mtumiaji wa mirungi yupo katika hatari ya kupata vidonda vya tumbo.

-         Kupungukiwa msukumo wa kufanya tendo la ndoa (low sex drive) na pia kuwahi kumaliza haraka na kutoweza kudumu kwenye tendo la ndoa kwa muda mrefu

-         Ukosefu wa haja kubwa (constipation)

-         Utumiaji wa muda mrefu husababisha ini kushindwa kufanya kazi,pia meno kubadilika rangi,kudhoofika,fizi kuuma na harufu mbaya mdomoni

-         Upungufu wa usingizi

-         Humpelekea mlaji kutawaliwa nayo(addiction)

-         Madhara ambayo bado kinamama walaji Mirungi hawajagundua ni kwamba mtoto anayezaliwa na mama mlaji Mirungi mara nyingi hukataa kunyonya titi la mama yake kwa sababu ladha ya maziwa inabadilika kwa ajili ya utumiaji wa madawa (pesticides) unaotumiwa na wakulima wa Mirungi kama inavyoeleza utafiti uliofanyika na Chuo Kikuu Cha Aden (Aden University).

-         Utafiti mwengine kule Ethiopia unatueleza ya kuwa mtoto wa mama mwenye kula Mirungi kwa wingi huwa hana uzito wa kawaida wakati wa kuzaliwa.

-         Ukosefu wa hamu ya kula chakula.

Saturday, August 23, 2014

TAMBUA MATUMIZI SAHIHI YA KONDOM

the hand of a young woman pulling a condom to prevent pregnancy from her jeans pocket - stock photocondom - stock photoCondom use icons - stock vector
 

Awali ya yote jamii inabidi ifahamu ukweli kuhusu matumizi sahihi ya kondomu kwasababu ninaamini watu wengi wanafikiri wapo katika njia sahihi ya kujikinga na maradhi mbalimbali kwa kutumia kondomu lakini badala yake wanakosea kutumia ipasavyo,hivyo kupata maambukizi ya maradhi hayo. Au unaweza kukosea kuitumia ukasababisha mwanamke kupata mimba, jambo ambalo halikua lengo lenu.

HATUA ZA KUTUMIA KONDOMU YA KIUME

-         Kwanza, kabla ya kununua angalia tarehe kama imeshaexpire au la! Pia kama kasha lake limetoboka. Usinunue!

-         Baada ya kununua ifungue taratibu kwasababu,kwa kadri unavyoivuta sana ndivyo inaweza kuchanika kwa wepesi

-         Ifungue kama ilivyoelekezwa katika pakiti yake

-         Wakati wa kuivaa shikilia sehemu ya mwisho (tip) na uache nafasi katika (tip) ya kondomu ambayo iko kwa ajili ya kushikilia shahawa wakati wa kujamiiana

-         Vaa kondomu kwenye uume uliosimama(erect penis)

-         Kama umekosea kuivaa, usivae tena bali uvue na kuitupa,kasha uchukue nyingine

-         Baada ya kujamiiana vua kondomu kwa kuvuta kutoka mwisho(tip) wakati bado uume ukiwa umesimama (erect)

-         Tumia kondomu nyingine kama unataka kuendelea

NB; wengine wanaamini kuvaa kondomu mbili au zaidi ndo inazuia maambukizi! La hasha! Vaa kondomu moja tu.

Na kumbuka kuwa matumizi ya kondomu hayazuii maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa asilimia 100.

Kwahiyo ;

1.  Epuka kufanya ngono zembe

2.  Kuwa mwaminifu na mpenzi mmoja uliye naye

Friday, August 22, 2014

JUA UZAZI WA MPANGO HAPA!!!!!!


 

Uzazi wa mpango ni kupanga au kuchagua ni wakati gani unapenda kuwa na mtoto,idadi,na upishano wa miaka kutoka mtoto mmoja hadi mwingine.

Zipo njia nyingi za kisasa za kupanga uzazi;

1.  Vidonge vya kumeza vyenye vichocheo vya aina mbili

2.  Vipandikizi(norplant)

3.  Njia za maumbile

4.  Vidonge vya kumeza vyenye kichocheo cha aina moja

5.  Kondomu

6.  Kufunga kizazi mwanamke

7.  Depoprovera

8.  Kufunga kizazi mwanaume

9.  Njia ya unyonyeshaji baada ya kujifungua

10.              Kalenda

TAHADHARI:

Thursday, August 21, 2014

MAMBO AMBAYO MAMA MJAMZITO ANATAKIWA KUWA MAKINI ANAPOYAONA

 
Mama mjamzito ni haki yake kupendwa na kulindwa kwasababu amebeba mtoto tumboni ambaye ni faidal kubwa sana katika jamii. Hivyo basi, ni lazima jamii sasa ibadilike na kuona umuhimu wa kwenda kucheki afya zao mara kwa mara hospitalini.
Kwa mama mjamzito,kuna baadhi ya mambo ambayo pindi anapoyaona asisubiri hata lisaa nyumbani,badala yake aende hospitalini haraka iwezekanavyo ili apate huduma kutoka kwa daktari na wahudumu wa afya sehemu husika.
MAMBO HAYO NI:
-         Kutokwa na damu sehemu za siri (vaginal bleeding)
-         Kutokwa na maji yanayotokana na kupasuka kwa chupa (vaginal discharge)
-         Kuwa na homa kali(kuchemka)
-         Kuwa na uchungu  kwa mimba yenye umri wa wiki 34
-         Kupungua kucheza kwa mtoto au kutocheza kabisa
-         Miguu kuvimba
-         Kichwa kuuma sana
-         Pia anapokuwa amefika hospitalini ,kama amepimwa pressure na ikawa zaidi ya 140/90 na zaidi,hiyo pia ni hali ya hatari
-         Kama pia mama amerukwa na akili wakati wa ujauzito afike hospitalini haraka iwezekanavyo
NB; KUMBUKA! Lengo ni ili

Wednesday, August 20, 2014

ELIMU KUHUSU UGONJWA WA EBOLA


 

Virusi vya ebola viligunduliwa hapo awali mwaka 1976 katika jamhuri ya kidemocrasia ya Congo ( Zaire) na Sudan. Ugonjwa wa ebola ulipewa jina hilo baada ya kugunduliwa huko Congo  kutokana na mto unaoitwa (Ebola river)  huko Congo.

Ugonjwa huu wa ebola unasababishwa na virusi vinavyojulikana kwa jina la Ebolavirus.

Ugonjwa huu unaenezwa kwa njia zifuatazo;

1.  Mgusano wa damu au utepetepe (body fluids) kutoka kwa mtu aliye na virusi vya ebola

2.  Mgusano wa vifaa vya hospitalini hasa sindano zilizohudumia mtu mwenye virusi hivyo pia vinaweza kusambaza ugonjwa huo

3.  Shahawa kwa mtu mwenye ebola pia zimeripotiwa kusambaza virusi hivyo vya ebola

4.  Pia mtu aliyefariki kwa ugonjwa wa ebola anaweza kupata virusi hivyo kama atagusa maiti hiyo bila kuvaa vifaa vya kujikinga.

5.  Shida pia ni kwa wahudumu wa afya ambao wanahudumia maelfu ya watu bila kujua yupi ni yupi mwenye ugonjwa huo bila kuvaa vifaa maalumu vya kujikinga

NB; Njia ya hewa haijagundulika kama inaweza kusambaza virusi hivyo,lakini  uchunguzi bado unaendelea .

DALILI ZA UGONJWA WA EBOLA

-         Katika hatua ya awali ya ugonjwa wa ebola, mgonjwa anakua na mafua yanayoambatana na uchovu,homa,kichwa kuuma,kuuma kwa viungo vya mwili,misuli na tumbo.

-         Kichefuchefu,kutapika damu, kuharisha damu ,na kuishiwa hamu ya kula

-         Dalili zingine kama,koo kukauka,kifua kuuma,kwikwi,kupata shida wakati wa kumeza na kupumua.

-         Pia mgonjwa anaweza kuota viupele mwilini.

NB; Tangu mtu aambukizwe virusi hivyo mpaka atakapoonyesha dalili,huwa inachukua siku 8 hadi 10.

TIBA;

Thursday, August 14, 2014

UMUHIMU WA KLINIKI KWA MAMA MJAMZITO


 

Kwa kawaida mama mjamzito anaanza kliniki na anatakiwa kuhudhuria mara nne kama hana matatizo yoyote. Hii ni kutokana na utaratibu uliowekwa na wizara ya afya na ustawi wa jamii. Wizara imeweka mambo ambayo mama mja mzito atatakiwa kupewa kama haki yake ikiwa na lengo kuu la kupunguza vifo vya mama na mtoto ambavyo hapo awali vilikua vingi sana.

Katika kutoa huduma hiyo ambayo ipo hata katika zahanati, kuna mambo ya msingi ambayo mama atapewa.

HUDUMA GANI ANATAKIWA KUPEWA????

1.  Huduma kama;kupima uzito,kupima presha,kupima wingi wa damu,kupima kama mtoto anacheza tumboni.

2.  Kumpatia mama vidonge vya kuongeza damu(folic asidi na feras sulfeti)

3.  Kupewa vidonge vya SP ili kumkinga na malaria

4.  Vidonge vya minyoo

5.  Sindano ya pepopunda

6.  Pia mama anatakiwa apewe ushauri kuhusu dalili za hatari,uzazi wa mpango,maandalizi ya kujifungua,magonjwa yatokanayo na kujamiiana na matumizi sahihi ya kondomu

7.  Pia anatakiwa kupimwa VVU,kaswende,grupu la damu

8.  Pia atapimwa tumbo

ATHARI YA KUTOPATA HUDUMA HIZO

Mama mjamzito asipopatiwa huduma hizo ana hatari ya;

-         Anaweza kupata matatizo ya presha( kifafa cha mimba)

-         Matatizo wakati wa kuzaa ambayo yanaweza kumpelekea mtoto kufa

-         Mtoto anaweza kuzaliwa njiti

-         Mtoto anaweza kuzaliwa akiwa na magonjwa mbalimbali

-         Pia mama anaweza kupoteza uhai wake.

KUMBUKA KATIKA MAMBO AMBAYO YANACHANGIA VIFO VYA MAMA WAJAWAZITO NA WATOTO NI KUKOSA HUDUMA THABITI ZA AFYA.

Tuesday, August 12, 2014

JE MAMA MWENYE VIRUSI VYA UKIMWI ANARUHUSIWA KUNYONYESHA?


 
Kwa kawaida mama anatakiwa kumnyonyesha mtoto kwa takribani mwaka mmoja hadi miaka miwili na kuendelea. Na katika miezi sita ya mwanzoni mama ni lazima amnyonyeshe mwanae bila kumpa kitu kingine chochote,hata maji ya kunywa hayaruhusiwi! Ndipo baada ya miezi sita mama anaruhusiwa kumuanzishia mtoto vyakula vingine kama uji wa lishe,maji nk.

Na ikumbukwe kuwa unapomuanzishia mtoto kitu kingine tofauti na maziwa ya mama katika miezi sita ya mwanzo,unamuweka mtoto kwenye mazingira ya kupata maambukizi ya bacteria na virus kutokana na umuhimu wa maziwa ya mama. Hii ni kutokana na tafiti zilizofanya na shirika la afya duniani (        WHO).

JE KWA MAMA ALIYEATHIRIKA???

Kwa mama mwenye virusi vya ukimwi anashauriwa kunyonyesha mtoto wake hadi mwaka mmoja tu,zaidi ya hapo mtoto ana hatari ya kupata maambukizi kwasababu ya ule msuguano wa mtoto anaponyonya. Atafuata utaratibu wa kawaida wa kunyonya tu kwa miezi sita ya mwanzo alafu hii mingine atamchanganyia kama kawaida kwa mwaka mmoja tu ndipo ataacha kumnyonyesha.

SOMA: UMUHIMU WA MAMA KUMNYONYESHA MWANAE


 

Mashirika ya afya pamoja na tafiti mbalimbali zilizofanyika duniani zimebainisha kwa kina sana juu ya umuhimu wa mama kumnyonyesha mtoto. Hii ni kwasababu, kutokana na utandawazi, kina mama wengi kutokana na majukumu ya kikazi hawanyonyeshi watoto wao, huku wakiwanywesha maziwa ya wanyama mfano ng’ombe au mbuzi.

Lakini na ijulikane kuwa maziwa ya mama yana virutubisho tofauti kabisa na ya ng’ombe au mbuzi, ya mama ni kwa ajili ya mtoto na ya ng’ombe ni kwa ajili ya ndama.

JE KUNA FAIDA GANI YA KUNYONYESHA?

1.  Yana kinga ya mwili kwa mtoto dhidi ya bacteria na virus wanaosababisha mtoto kuharisha,homa ya mapafu(pneumonia),homa ya uti wa mgongo

2.  Maziwa ya mama yana virutubisho vyote muhimu vinavyomjenga mtoto kiukuaji,yaani,protini,carbohydrate,mafuta,vitamin,madini,na maji.

3.  Pia ukimnyonyesha mtoto wako unamjenga kisaikolojia,tafiti nyingi zimetanabaisha tofauti ya watoto walionyonyeshwa na ambao hawakunyonya.

4.  Maziwa ya mama yana joto ambalo linahitajika kwa mtoto

5.  Maziwa ya mama hayana contamination ya bacteria hasa akinyonyesha kwa usafi