Sunday, July 27, 2014

UMUHIMU WA CHANJO KWA WATOTO CHINI YA UMRI WA MIAKA 5

Chanjo ni kemikali anayopewa mtu ili kumjengea kinga ya mwili dhidi ya magonjwa. Chemikali hiyo inaweza kuwa katika mfumo wa matone,vidonge au sindano. Katika uchunguzi uliofanywa na wanasayansi duniani ni kwamba watoto wengi ambao aidha hawajapata au kukamilisha chanjo huwa wanasumbuliwa na magonjwa mbalimbali kutokana na kukosa chanjo dhidi ya ugonjwa huo.

Kwa hapa kwetu Tanzania tuna program mpya ya kutoa chanjo kwa watoto ijulikanayo kama (IVD)-Immunization and Vaccination Development ambayo mwanzoni ilikua inaitwa ( EPI) Expanded Programme of Immunization.

NAMNA ZINAVYOTOLEWA

-         Siku anapozaliwa

-         Akiwa na wiki 6 au mwezi mmoja na nusu

-         Akiwa na miezi miwili na nusu

-         Akiwa na Miezi mitatu na nusu

-         Akiwa na Miezi tisa hadi miaka mitano kila baada ya miezi sita

UMUHIMU WA HIZI CHANJO

-         Zinamkinga mtoto kupata maambukizi ya magonjwa kama kifua kikuu,homa ya mapafu,kifaduro,tetenasi,polio,tetekuwanga,kuharisha,surua,homa ya uti wa mgongo,ukavu macho.

  Kumbuka mtoto asipopata chanjo hizo yuko katika hatari ya kupata maambukizi hayo na mwisho wake ni mbaya. Hivyo mpeleke mtoto wako kliniki ili apatiwe chanjo kama hajapatiwa na ana umri chini ya miaka mitano.

  CHANJO NI HAKI YA MTOTO!!!!!!!

 

IMEANDALIWA NA:  BWAMBO HEALTH FARM

KWA USHAURI NA MAONI:WASILIANA NASI KWA NAMBA:  +255 716648735  AU +255 688648735

KWA TAARIFA ZAIDI TEMBELEA UKURASA WETU WA FACEBOOK NA “LIKE” PAGE YETU

BWAMBO HEALTH FARM TUNAJALI AFYA YAKO

 

No comments:

Post a Comment