Tuesday, July 15, 2014

TATIZO LA UTASA


 

Shirika la afya duniani limetoa maana ya utasa kuwa ni hali ya mwanamke kutoweza kushika/kupata mimba.hali hiyo inaitwa utasa  pale ambapo mke na mume wanakaa takribani muda wa miaka miwili bila kupata mtoto ili hali wanajamiiana mfululizo kwa lengo hilo la kupata mtoto bila ya kutumia kinga yoyote.

AINA ZA UTASA

Kuna aina mbili za utasa;

1. Utasa wa awali (primary infertility),huu ni ule ambao mke na mume hawajawahi kupata mtoto.

2. Utasa wa baadae(secondary infertility),na huu  ni ule ambao mke anashindwa kupata/kushika mimba baada ya kuzaa hapo awali.

VISABABISHI VYA UTASA

Visababishi hivi vimegawanyika katika makundi mawili;

1.   Visababishi kwa mwanamke

2.   Visababishi kwa mwanaume

 

SABABU ZA UTASA KWA MWANAMKE

-         Kuziba kwa mirija  ya uzazi,hii inasababishwa na magonjwa kwa kitaalamu tunaita PID(Pelvic Inflammatory Diseases) ambayo yanaweza kujumuisha mirija ya falopia,uterus na ovary(mayai ya uzazi)

-         Tatizo la kutopata mzunguko wa kawaida wa hedhi,,hii inaweza kusababishwa na magonjwa mengi tu,kwa kitaalamu tunaita PCOS(polycystic ovary syndrome) ambapo katika kiwanda cha kutengenezea mayai ya uzazi kunakua na uvimbe ambao ndani yake kuna maji hivyo kusababisha mayai kushindwa kutengenezwa vizuri na hata kama yakitengenezwa usafirishwaji wakeunakua ni mgumu kutokana na uvimbe/vimbe hizo.

-         Umri,tunajua mwanamke anakua na uwezo wa kuzaa kwa wastani wa miaka kuanzia 11 anapo balehe hadi 40 au 45,zaidi ya hapo ni ngumu kwa mama huyo kupata mimba kwasababu mayai yanakua yamekwisha na kiwanda cha kuzalisha mayai hakitengenezi tena.

-         Upasuaji (operation) ya kufunga kizazi,kama mama ameshawahi kufunga kizazi (tubal ligation) hawezi tena kupata mimba kwasababu yai haliwezi kupita na kufikia uterus ambapo mimba hutungwa.

-         Nk

SABABU ZA UTASA ZINAZOTOKANA NA MWANANUME

-         Kutoa shahawa/mbegu kidogo sana,nah ii husababishwa na mambo mengi kama magonjwa ya mfumo wa uzazi wa mwananume,baadhi ya madawa ya kulevya,matatizo ya kihomoni,na mionzi pia.

-         Kutoa mbegu ambazo hazina uhai,hii ni kutokana na ukweli kwamba mwanaume anaweza kutoa mbegu ambazo zimekosa uhai yaani (nucleus) hii inaweza kusababishwa na magonjwa,madawa,mionzi na pia yaweza kurithiwa.

-         Nk.

USHAURI; KUPIMA AFYA YAKO NI MUHIMU SANA,USISUBIRI HADI UWE NA MATATIZO,,,NA KAMA UNA HILO TATIZO NENDA HOSPITALINI ILI UCHEKI AFYA YAKO.

IMEANDALIWA NA; BWAMBO HEALTH FARM TEAM www.bwambohealth.blogspot.com

CONTACTS; +255 716648735

                       +255 688648735

Like our page on facebook

 

-          

No comments:

Post a Comment