Monday, July 21, 2014

TATIZO LA KUHARISHA KWA WATOTO


 
Shirika la afya duniani limetoa maana ya kuharisha kwamba ni kupata choo zaidi ya mara tatu au nne kwa siku.watoto wadogo hasa chini ya miaka mitano mara nyingi wanakumbwa na tatizo la kuharisha ambalo huwapelekea kuwa dhaifu sana na hata wengine kupoteza maisha.

KWANINI WATOTO HAWA WANAHARISHA?

Hii ni kwa sababu ya uchafu kutoka kwa mama pale ambapo atamnyonyesha mtoto bila kusafisha  matiti yake kwa maji safi,na pia kunawa mikono kabla na baada ya kumnyonyesha mtoto. Uchunguzi umebainisha kuwa watoto wanaharisha kutokana na virus wanaoitwa rotavirus ambao hutokana na uchafu.Na mara nyingi wanaharisha majimaji.

DALILI

-         Mtoto anakuwa na hamu ya kunywa maji sana

-         Mtoto anakuwa na ukavu macho,yani hata akilia hatoi machozi na macho yanazama

-         Anakua hatulii,anahangaika sana au kulialia

-         Anachoka sana na anaweza kupoteza fahamu

-         Ngozi yake inakua kavu

 

NINI KIFANYIKE?

-         Mtoto apelekwe katika kituo cha afya au hospitalini mara baada ya kuanza kuharisha; kwasababu kuharisha kunampelekea mtoto kuwa dhaifu kutokana na kupoteza maji mengi ya mwili.

 

NAMNA YA KUZUIA

-         Mama ahakikishe mtoto ananyonya katika mazingira safi,yaani mama awe ananawa mikono kabla na baada ya kunyonyesha,pia asafishe matiti yake kwa maji safi na salama kabla na baada ya kunyonyesha.

-         Mama amuweke mtoto katika usafi wakati wote ili kuzuia magonjwa mengine.

-         Hakikisha mtoto anapatiwa chanjo za aina zote.

 

 

IMEANDALIWA NA ; BWAMBO HEALTH TEAM

KWA USHAURI NA MAONI WASILIANAN NASI  KWA ;   +255 716648735  au  +255 688648735

Like page yetu ya facebook kwa habari zaidi. Andika Bwambo Health FARM/Facebook  kisha like.


 

 

No comments:

Post a Comment