Wednesday, July 30, 2014

HALI HATARISHI KWA MTOTO (DANGER SIGNS)

sick child : Mother checking temperature of sick daughter by hand Stock Photo
 
Kuna utofauti mkubwa kati ya watoto na watu wakubwa (adults), tena watoto wachanga ambao bado hawawezi kuongea ni vigumu kujua wanasumbuliwa na kitu gani. Lakini zipo dalili au hali hatarishi ambazo ukiziona ni lazima umpeleke mtoto katika hospitali au kituo cha afya kilicho karibu nawe. Ikitokea mzazi anapuuzia hali hiyo mtoto anaweza kupoteza uhai wake kwa muda mfupi sana.

DALILI ZA HALI HATARISHI

1.  Kupumua kwa shida au kukosa hewa( kukosa kupumua)

2.  Kubadilika rangi na kuwa wa bluu

3.  Mapigo ya moyo kwenda mbio kuliko kawaida

4.  Kupoteza fahamu

5.  Degedege

6.  Dalili za kuishiwa maji ya mwili kwa mtoto anayeharisha ( mfano,macho kuzama,kulegea,ngozi kuvutika)

Uonapo dalili hizo tafadhali mpeleke mwanao kituo cha afya mara moja.

OKOA MAISHA YA MTOTO,TIMIZA NDOTO ZAKE!!!!!!!

Ref; WHO

IMEANDALIWA NA: BWAMBO HEALTH FARM

KWA  SWALI,USHAURI NA MAONI WASILIANA NASI KWA: +255 716648735 AU +255 688648735


Tembelea facebook page yetu na ‘like’ kwa habari nzuri za kukujenga za kiafya

www.bwambohealth.blogspot.com tunajali afya yako.

No comments:

Post a Comment