Thursday, April 17, 2014

ZITAMBUE HATUA ZA UKIMWI-KUPIMA NI MUHIMU


Je, kuna hatua ngapi za ugonjwa wa VVU/UKIMWI na dalili zake ni zipi?

Kwa mujibu wa uanishaji uliofanywa na wataalamu wa Shirika la Afya Duniani yaani WHO, kuna hatua kuu nne za ugonjwa wa VVU/UKIMWI ambazo ni:

1. Hatua ya kwanza au maambukizi ya mwanzo ya HIV. Hatua hii huwa ni ya muda wa wiki nne na ni asilimia 20 tu ya watu wenye maambukizi ya VVU walio kwenye hatua hii ambao hupata dalili na viashiria vikali vya ugonjwa huu, lakini mara nyingi  madaktari hushindwa kutambua kama mgonjwa amepata maambukizi ya virusi vya Ukimwi kutokana na dalili na viashiria vyake kufanana sana na dalili za magonjwa mengine. Mgonjwa aliye katika hatua hii ya kwanza ya maambukizi ya VVU huweza kuonesha dalili na viashiria kama vile kuvimba tezi, kupatwa na homa kali, kuumwa koo, kujihisi mchovu, kujihisi maumivu sehemu mbalimbali mwilini kutokwa na vipele mwilini,kutapika, kuharisha au kuumwa tumbo. Mgonjwa anayepata dalili na viashiria hivi tunasema kwamba amepata "Acute HIV infection/Acute HIV retroviral infection au seroconversion illness." Dalili hizi hutokana na mwili wa mtu mwenye maambukizi ya VVU kuanza kutengeneza kinga dhidhi ya VVU.

2.Hatua ya Pili ni isiyokuwa na dalili au Clinically Asymptomatic Stage.

Katika hatua hii ambayo inaweza kudumu kwa muda wa miaka 10, mgonjwa haoneshi dalili au viashiria vyovyote vile isipokuwa anaweza kuwa na tezi zilizovimba. Kiwango cha VVU kwenye damu hupungua sana lakini mgonjwa anaweza kuambukiza mtu mwingine yoyote na vipimo vya Ukimwi vina uwezo wa kutambua uwepo wa maambukizi ya VVU katika damu. Tafiti mbalimbali zimeonesha kwamba, VVU katika mwili huwa bado vinazaliana na hukimbilia na hujificha kwenye tezi. Kutokana na kujificha kwake katika hatua hii, kipimo cha kupima wingi wa virusi vya ukimwi au Viral load test katika mwili hutumiwa sana ili kuweza kutambua uwepo wa VVU. Kipimo hiki pia husaidia katika kumpangia mgonjwa tiba yake.

3. Hatua ya Tatu yenye viashiria au Symptomatic HIV infection. Katika hatua hii kutokana na kuongezeka kwa wingi VVU katika mwili, kinga ya mwili huzidi kudhoofika suala linalosababisha mambo kadhaa. Kwanza ni tezi na tishu zilizoathiriwa na VVU huharibika kutokana na maambukizi ya muda mrefu. Pili VVU hubadilika badilika na kuwa na uwezo zaidi wa kuathiri tishu na sehemu mbalimbali za mwili na hata kuziua au kuharibu seli zinazokinga mwili kutokana na maambukizi, zinazojulikana kama T helper cell, seli T saidizi. Pia mwili hushindwa kumudu uharibifu wa seli T saidizi na kushindwa kuzalisha seli nyingine mpya.

4.Hatua hii ya nne ni ile ambayo tayari virusi vya ukimwi vimeanza kuathiri sehemu mbalimbali ya mwili kwa kuuweka mwili katika hali ambayo ni rahisi kwa magonjwa yanayotokana na upungufu huo wa kinga mwilini kuattack.

Baadhi ya magonjwa nyemelezi yanayoweza kumpata mtu mwenye ugonjwa VVU/UKIMWI ni pamoja na

- . Magonjwa ya mfumo wa kupumua kama vile ugonjwa wa homa ya mapafu, kifua kikuu (TB) na  saratani aina ya Kaposi's sarcoma.

-   Magonjwa ya mfumo wa chakula kama vile Cryptosporidiosis, fangasi za Candida, Cytomegolavirus (CMV) na Isosporiasis.

-   Magonjwa ya mfumo wa fahamu kama vile Cytomegolavirus, Toxoplasmosis, Cryptococcosis, saratani ya Non-Hodgkin lymphoma,Tuberculoma.a

-   Magonjwa mbalimbali ya ngozi kama vile Herpes simplex, Kaposi's sarcoma (saratani ya ngozi) na Varicella Zoster (mkanda wa jeshi].

 

No comments:

Post a Comment