Sunday, December 15, 2013

EPUKA CHUMVI ZA MEZANI KIAFYA


Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha kuwa mwaka 2005 peke yake palitokea vifo vya watu milioni 17.2 duniani kwa magonjwa ya moyo.

Hii ni  asilimia 30 ya vifo vyote duniani huku kina mama wakiongoza kwa kufa zaidi. Pia, kila mwaka katika vizazi hai 1,000, watoto wanane huzaliwa na matatizo ya moyo katika Tanzania. Takwimu zinaonyesha kuwa kati ya asilimia 20-30 ya watu wanaugua magonjwa ya moyo.

Inakadiriwa kuwa ifikapo  mwaka 2020 magonjwa ya kuambukiza yatakuwa na uwiano sawa na magonjwa yasiyoambukiza, yaani asilimia 50 kwa 50 kwa nchi za Afrika ambako kwa sasa vifo vingi husababishwa na magonjwa ya kuambukizwa kama vile, malaria, kifua kikuu na Ukimwi.

Hii ni kutokana na maendeleo ya kiuchumi ambayo huambatana na magonjwa yasiyoambukiza kama vile, shinikizo la damu, shambulizi la moyo, figo, kiharusi na kisukari. Siku ya magonjwa ya moyo duniani  inakwenda sambamba na matumizi ya kiungo muhimu kiletacho ladha katika chakula, yaani chumvi. 

Chumvi ni kitu chenye kihistoria duniani, tangu miaka milioni iliyopita chumvi imekuwapo na kutumika duniani.

Chumvi ni moja ya vitu vilivyomo katika maji ya baharini, baada ya maji kuwa mvuke baada ya kupata joto, chumvi hubaki kama vichangarawe vidogovidogo ambavyo huvunwa na kutumika.

Ukipita majumbani, hoteli zote, migahawa, minadani, matamasha na mitaani vijiwe vya nyama choma utashuhudia ulaji mkubwa wa chumvi. Watu hujimiminia chumvi katika chakula hata kama chakula hicho kina chumvi. Wengi wao hawafahamu kama ulaji chumvi kwa mtindo huo ni hatari kwa afya zao.

 

No comments:

Post a Comment